Hamjambo wadau?
Nyingine hiyo ya Kanga kutoka Kibua Designs
Wenzangu na mie inafaa sana kwa kitchen party
***
Haya kina kaka, kina baba
Ya kitenge hiyo
Wallet safi, kutoka Kibua Designs
Imetengenezwa kwa kitenge
Ni nzuri sana, ina ubora, inadumu kuliko hata hiyo ya ngozi uliyokua nayo
Hamjambo!
Leo tuone jinsi ya kutengeneza chachandu
Mahitaji:
Pilipili kali (inayowasha)
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Sukari (sio lazima)
Kitunguu saumu
Kitunguu maji
Tangawizi
Hoho
Nyanya
Mliojaaliwa neema za Mungu mpo?
Mambo yenu haya
Tizama post hii ya kitenge
Kimojawapo ndio kimetoa nguo hii
Habari wadau!
Hope mko poa
Ya kitenge hiyo toka kwangu
Siku nyingi sijatupia haya mambo sababu ratiba zilikua zinabana
Bonyeza chini hapo kuona swaga zaidi
Habari!
Natumai muwazima wa afya njema kabisa
Ya kwangu ya kitenge
Ni kikoti(Blazer) cha kawaida tu
Manjonjo(details) mgongoni hapo
Kuna malinda ya uongo na kweli
Umeipenda?
Nitafute
kibuafashions@gmail.com
Usisahau Kunifollow
***
Habari wadau!
Ya kitenge hii toka kwangu,
Ni skirt na blauzi za kawaida kabisa
Skirt kimtaa tunaita "A shape", mbele ina mipasuo miwili, usawa wa goti kushoto na kulia
Lakini kwenye picha hapa hainekani vizuri
Na kwa nyuma ni pande mbili za kawaida
Habari zenu wapendwa!
Mko poa?
Nyingine tena ya kitenge toka kwangu
Evening Kitenge Dress
Waweza tupia kivazi hichi kwenye mtoko wa jioni au kwenye sherehe kama kitchen party, send off au harusi
Bonyeza chini hapo kwa picha zaidi
Aje!
Mko poa?
Nyingine hii ya kitenge kutoka kwangu
Ni sketi ya belt kubwa, malinda ya kuvuta na mifuko
Zipu na vifungo, nimeweka nyuma
Ni rahisi sana kutengeneza hii sketi, sababu ya muda nashindwa kupost picha na video za jinsi ya kutengeneza nguo simple ambazo wewe mdau unaweza ukajitengenezea ya kwako hapo nyumbani
Naahidi nitakapopata muda nitapost tutorial za kushona nguo simple
Sketi kama hii haiitaji uwe mtaalamu sana wa kushona, hata yule ambaye ana utaalamu kidogo wa kushona anaweza akashona mtindo huu
Top nimeiremba kidogo na ua la kitenge ambacho nimetumia kwenye sketi
Bonyeza hapo chini kuona picha zaidi
Mahitaji:
Nyama/Beef
Soya sauce
Tangawizi
Kitunguu saumu
Limao/ndimu(sio lazima)
Mafuta ya kupikia
Kitunguu maji
Nyanya
Hoho
Karoti
Chumvi
Nyama/Beef
Soya sauce
Tangawizi
Kitunguu saumu
Limao/ndimu(sio lazima)
Mafuta ya kupikia
Kitunguu maji
Nyanya
Hoho
Karoti
Chumvi
Njia:
Anza kwa kukatakata nyama, kisha isafishe vizuri. Kisha changanya nyama pamoja na tangawizi na kitunguu saumu ambavyo utakua umeviandaa kwa kuviponda au kuvichop. Ongezea na soya sauce kisha iache kwa muda wa kama dakika 30 mpaka 45. Hii itasaidia nyama kuiva haraka
Wakati unasubiria nyama iendelee kuchanganyika na viungo vizuri, tumia muda huo kuandaa mbogamboga zako ambazo zitaenda sambamba na pishi hili la rainbow beef
Anza kwa kukatakata nyama, kisha isafishe vizuri. Kisha changanya nyama pamoja na tangawizi na kitunguu saumu ambavyo utakua umeviandaa kwa kuviponda au kuvichop. Ongezea na soya sauce kisha iache kwa muda wa kama dakika 30 mpaka 45. Hii itasaidia nyama kuiva haraka
Wakati unasubiria nyama iendelee kuchanganyika na viungo vizuri, tumia muda huo kuandaa mbogamboga zako ambazo zitaenda sambamba na pishi hili la rainbow beef
Baada ya mahitaji yako yote kuwa tayari, andaaa jiko lako utakalotumia kupikia pishi lako, angalia moto usiwe mkali kwan utasababisha chakula chako kutoiva vizuri
Weka sufuria yako jikoni, ikishapata moto weka mafuta ya kupikia kiasi
Mafuta yakishapata moto, weka nyama na ukoroge koroge mpaka itakapoiva
Nyama ikishaiva vizuri weka mbogamboga zako, anza na vitunguu maji, karoti, hoho kisha malizia na nyanya. Geuza kwa sekunde kadhaa mpaka uone mboga mboga zimechanyanyika vizuri na nyama. Kisha tia chumvi kwa ajili ya taste.
Usiache mboga mboga zikaiva sana kwani hazitaleta maana ya jina la pishi hili. Kwa kuwa ni rainbow beef lazima mboga mboga zionekane vizuri na rangi zake. Pia katika mahitaji yako waweza kuongezea red pepper, yellow pepper, uyoga nk. kadiri ya mapenzi yako. mimi kwa leo nimetumia mahitaji haya unayoyaona kwenye picha
Baada ya hapo pishi lako linakua tayari kwa kuliwa.
Unaweza kuandaa na chakula chochote unachopenda, kama wali, tambi, macaroni, ugali, viazi nk.
Si vibaya kukawa na kinywaji pembeni kama juice au soda
Na hili ndio pishi letu la leo rainbow beef. Unaweza kuandaa wewe mwenyewe hapo nyumbani kwa kufuata njia hizi nilizozielezea
Una swali, maoni, ushauri?
Niandikie kibuafashions@gmail.com
***
Violet
Hivi unajua kuwa unaweza kuwa mrembo kwa kutumia vitu vya asili tu?
Ndio inawezekana! Wengi wetu tumekariri kwamba, ili uwe mrembo na mwenye muonekano wa kuvutia machoni pa watu, basi ni lazima utumie vipodozi vya madukani, vyenye kemikali za kila aina. Tena vingine vina kemikali za sumu. Na vipodozi hivi vinauzwa kwa bei ghali kweli. Na wakati mwingine usipate hata yale matokeo uliyokuwa unategemea. Unakua umepoteza pesa na umezidi kuharibu muonekano wako wa asili.
Kwa nini uendelee kupoteza pesa na muda kwa vipodozi ambavyo havikupi matokeo stahili.
Wakati kuna vitu vya asili ambavyo vinaweza kukusaidia ukawa na muonekano mzuri, tena kwa gharama nafuu
Sasa leo nitawaeleza maajabu ya nazi katika urembo
Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza ikatumika kama scrub kwa ngozi yako
Fuata hatua hizi hapa chini ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako kuwa na muonekano mzuri
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini kwa leo nitaelezea namna ya kuitumia kwa uso wako
Fuata hatua hizi hapa chini ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako kuwa na muonekano mzuri
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini kwa leo nitaelezea namna ya kuitumia kwa uso wako
Weninge huwa wanachanganya nazi pamoja na asali, limao, tangawizi, nk. Hii ninayoielezea hapa haijachanganywa na kitu chochote kile. Ni nazi pekee
Nini cha kufanya:
Nini cha kufanya:
* Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri. Ili upate matokeo mazuri jitahidi kuikuna taratibu ili itoke laini
* Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa(medicated soap)
*Kausha uso wako kwa taulo safi
*Baada ya uso wako kuwa mkavu, chukua ile nazi yako uliyokuna tayari, taratibu anza kusugua usoni kwa dadika kama 3 mpaka 5
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20
*Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida
*Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote
Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yani mara 1 kwa siku. Amini nakuambia utapata matokeo mazuri
Ni hayo tu niliyowaandalia siku ya leo wapendwa wangu
Kama una swali, maoni au ushauri
Niandikie kibuafashions@gmail.com
Pia kama una chochote kizuri cha kushare nasi, usisite kuniandikia
Uwe na siku njema mdau
***
Violet
Mahitaji:
Mchele
Choroko
Tui la nazi
Chumvi
Maji
Njia:
Chambua mchele kwa kutoa taka taka zote kisha uoshe vizuri ikiwezekana pembua ili kuondoa mawe kama mchele wako utakua na mawe
Chambua choroko na kisha zioshe vizuri na zichemshe kidogo, zisiive sana kwani zitalainika wakati unapoendelea kupika wali. Kwahiyo uwe makini hapa choroko zisiive
Kuna nazi yako uliyoiandaa
Pasha maji yawe ya uvuguvugu kidogo kwa ajili ya kuandalia tui. Ukitumia maji baridi tui halitoki vizuri, tui la kwanza(tui bubu) liweke pembeni kwani litatumika baadae kadiri unavyoendelea kupika
Endelea kuchuja tui la pili au na la tatu mpaka upate kiasi cha tui linalohitajika kwa pishi lako
Baada ya kuandaa tui lako tayari, weka kwenye sufuria ambayo utatumia kupikia pishi lako
Ongezea na choroko humohumo kwenye tui la nazi
Koroga koroga tui ili lisikatike
Baada ya tui kuchemka, ongezea chumvi na mchele. Koroga kidogo kisha funika ili wali wako uendelee kuiva taratibu
Angalia moto usiwe mkali, uwe wa wastani ili chakula chako kisiungue
Baada ya muda maji yatakua yamekaukia kwenye chakula chako, chukua lile tui bubu ulilokamua mwanzo, ongezea kwenye chakula chako kisha funika
Baada ya dakika kadhaa angalia chakula chako kama maji yatakua yamekaukia geuza chakula chako kisha funika tena
Kisha hapo utakua unageuza geuza chakula chako mpaka uhakikishe kimeiva
Chakula chako kikiiva kitakua na muonekano huu
Hapo kitakua tayari kwa kuliwa
Unaweza kuandaa na mchuzi wa kusindikizia chakula chako, kama mchuzi wa nyama, samaki, salad au ukiamua mbogamboga za majani yote sawa.
Lakini pia unaweza kula hivihivi kwa kuwa hapo tayari ni wali na mboga
Pia unaweza ukaandaa na kinywaji chochote
Una swali, maoni, ushauri?
Au una pishi ungependa kushare nasi
Niandikie kibuafashions@gmail.com
***
Violet