Habari wadau.
Natumai mlikua na jumapili njema. Tumshukuru Mungu kwa kutujalia pumzi maana kuna wengine hawajaiona siku ya leo. Wameshatangulia mbele za haki.
Tukiachana na hayo, leo nimewaletea kivazi hiki cha satin.
Hiki kivazi chavaliwa kwenye shughuli. Send off party sawa, sherehe ya harusi poa, hata kwa red carpet unaweza kutupiamo.
Pia vazi hili laweza valiwa na bi harusi mtarajiwa kwenye send off party yake.
Au kwa maids wa bi harusi, halichagui kwa sababu lipo simple sana.
Rangi iliyotawala hapo ni peach na rangi mnogesho light blue. Yenyewe imetumika kidogo tu kunogesha nguo. sio lazima kuvaa nguo yenye marangi mengi, inachusha. sio vibaya siku moja moja ukatokelezea simple kama hivi. inapendeza sana
Ni hayo tu kwa leo wapendwa wangu
Mbarikiwe sana
Kibua V
xo...
***
Habari wadau
Natumaini muwazima popote pale mlipo
Nyingine hii ya BATIK kutoka kwangu. Nimekuwa nikiwaletea sana style za kubana bana lakini leo nimeamua niwatupie hii ya solo. Ubunifu hapa sana sana uko kwenye shingo na kwenye mikono. Vingine vya kawaida sana tumeshazoea kuviona.
Unasemaje kuhusu mlipuko wa leo?
Una maoni? Mlipuko umekuvutia?
Usisite kutoa maoni, kwani maoni yako yana mchango mkubwa sana.
Pia usisahau kunifollow GFC, twitter na facebook kisha toa comment yako ili ushinde zawadi ya BATIK
bonyeza HAPA ili kushiriki kwenye mchakato
Kibua V
***