Weekend ilikua vipi wadau?
Natumai ilikua poa.
Natumai ilikua poa.
Mimi kwangu ilikua poa sana, namshukuru Mungu.
Nawatakia wadau wote jioni njema, iwe ya utulivu.
Mimi penda sana nyinyi
xoxo
***
So, jioni nilitokelezea hivyo, nikatupia blue skin jeans, wengine wanaita model, poa tu vyovyote utakavyoiita mradi tunaenda sambamba. Juu nikatupia kitu cha brown sweater. Simple & comfortable
Then, tukatoka marafiki zangu kwau ajili ya chakula cha jioni, tukala, tukanywa, tukafurahi. Pia nilikata keki. Na story ndio ikaishia hapo.
Napenda kuwashukuru wapendwa wote walionikumbuka katika siku yangu hii kubwa, walioniwish happy bday, walioniletea zawadi, kadi, bila kuwasahau mafans wangu wa facebook, nawashuru sana.
Nawapenda sana na ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu awabariki, awazidishie baraka tele, awape kila jema, awafanyie wepesi katika kila jambo na awaongezee katika kile mlichokitoa kwa ajili yangu.
Mungu awabariki sana
With love,
Violet
Fin
***
Today is my birthday and all I can say is that,
Thank you, God, for giving me another year of life.
Thank you for all the people who remembered me today
by sending cards, and letters, gifts and good wishes.
Thank you for all the experience of this past year;
for times of success which will always be happy memories,
for times of failure which reminded me of my own weakness and of my need for you,
for times of joy when the sun was shining,
for times of sadness which drove me to you.
Forgive me
for the hours I wasted,
for the chances I failed to take,
for the opportunities I missed this past year.
Help me in the days ahead to make this the best year yet,
and through it to bring good credit to myself,
happiness and pride to my loved ones,
and joy to you.
Thank you for all the people who remembered me today
by sending cards, and letters, gifts and good wishes.
Thank you for all the experience of this past year;
for times of success which will always be happy memories,
for times of failure which reminded me of my own weakness and of my need for you,
for times of joy when the sun was shining,
for times of sadness which drove me to you.
Forgive me
for the hours I wasted,
for the chances I failed to take,
for the opportunities I missed this past year.
Help me in the days ahead to make this the best year yet,
and through it to bring good credit to myself,
happiness and pride to my loved ones,
and joy to you.
AMEN.
Happy BDay to me!
Habari zenu wadau.
Hiyo ya kwangu nyingine, nimeamua kuiita shining star kwa sababu ya kitenge chenyewe kilichotumika kina nyota nyota. Kama tujuavyo nyota zikiwa angani zinang'aa kwahiyo nikaona sio vibaya nguo hii nikaipa heading ya shining star
Ukitizama vizuri maua ya kitenge hicho utagundua
Naomba nisiwachoshe kwa maneno mengi, kwani leo ni furahi day "friday" naamini wengine wameshaanza weekend.
Niwatakieni nyote weekend njema yenye amani, upendo na utulivu wa kutosha.
xoxo
***
Me, Myself n I
Hivi unajua kwamba kanga
nayo yaweza fanya maajabu katika fashion. Kwanza kanga hazina gharama
sana, kama vitenge. Hata yule mpenda mitindo wa kipato cha chini kama
mimi hapa anaweza kununua kanga na akadesign anavyojua yeye, mwisho wa
siku akatokelezea fresh.
Ukipata designer mzuri akakupangia yale maua ya kanga vizuri sina shaka utapendeza
Tatizo
la kanga hazina mapana makubwa, kwahiyo mitindo yake mara nyingi inakua
simple. Labda kama utataka mtindo wa makorokoro utalazimika kununua
doti zaidi ya moja.
Kama
mimi hapa nimedesign kamtindo simple, na naamini nimependeza. Hiki
kivazi naweza hata vaa ofisini, au mnasemaje wadau wangu?
Unaujua mpingo?
Basi huu ni mti unaopatikana hapa nchini kwetu Tanzania. Ni mti maarufu sana katika sanaa ya uchongaji. Mpingo hutumika kuchonga vitu mbalimbali kama vinyago vya kupamba majumbani, maofisini na sehemu nyingine tofauti tofauti kulingana na muhusika anavyopenda, Vinu vya kutwangia viungo mbalimbali, nk.
Lakini mpingo pia hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali za urembo, kama hapo juu pichani, ni hereni na bangili zilizotengenezwa kwa mti wa mpingo.
Hereni na Bangili hizi ni nzuri sana, kwanza zinadumu kwa muda mrefu kwa sababu mti uliotumika kutengeneza bidhaa hizi ni mti mgumu sana, kwahiyo hazivunjiki kwa urahisi. Pili hazipitwi na wakati, kwasababu mara zote vitu vya asili na kitamaduni huwa vinapendwa
Kama zimekuvutia tafuta yako utupiemo uone jinsi utakavyopendeza.
Ni hayo tu niliyokuandalia kwa siku ya leo. Nawatakia wadau wote weekend njema ya amani, upendo na utulivu wa hali ya juu.
Nawapenda sana
xoxo
***