mapishi

MAKANDE YA MBOGAMBOGA

7/20/2013Violet Kibua


Mahitaji:
Mahindi yaliyokobolewa
Maharage
Hoho
Karoti
Kitunguu
Chumvi
Tui la nazi
Njia:
 Anza kwa kuandaa mahindi na maharage kwa kuyachambua na kuyaosha vizuri
Kisha weka katika chombo utakachotumia kupikia, halafu bandika jikoni
Kwakuwa mahindi na maharage yanachukua muda mrefu kuiva, ni muhimu kuweka maji ya kutosha
Na ukiona maji yamekaukia na bado mchanganyiko wako haujaiva vizuri, basi ongeza maji kiasi
Na maji hayo ni vizuri yawe ya moto au uvuguvugu
Andaa mboga mboga zako ambazo ni hoho, karoti na kitunguu, kwa kuvikata vipande vidogo vidogo
Baada ya mchanganyiko wako wa mahindi na maharage kuwa umeiva ongeza chumvi kiasi, 
Wakati huohuo ongezea na mbogamboga ulizoziandaaAcha kwa muda kidogo ili mbogamboga zipate kuiva, lakini angalia zisiive sana mpaka zikalainika

Andaa tui la nazi kwa kukamua tui la kwanza na pili 
Utaanza kwa kuweka tui la pili, likishachemka kidogo utamalizia kwa kuweka tui la kwanza au tui bubu
Utaacha tui lichemke kwa muda kidogo ili lipate kuiva
Baada ya hapo chakula chako kipo tayari kuliwa

 

Maoni, ushauri au una pishi unataka kushare nasi
Niandikie
kibuafashions@gmail.com

***

You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form