27.4.15

LONG KITENGE DRESS

Habari wadau! 

Nyingine hii toka kwangu. Kitenge cha nyota nyota. Gauni ni ya malinda box. Ukitizama vizuri picha utaona, malinda box yapo mbele na nyuma pia. Hapo tumboni kuna belt la kishkaji. Pia vazi hili limetumia vitenge viwili kwa maana kwamba, kitenge ni design moja cha nyotanyota lakini rangi mbili tofauti, juu njano na chini pink. 

Gauni kama hii pia nilishawahi post HAPA lakini kuna tofauti kidogo tu shingoni.
Natumai mtaipenda. Kuona picha zaidi, bonyeza hapo chini

21.4.15

BATIK PEPLUM TOP

Habari wadau! Nyingine hii ya batiki toka Kibua Designs ukitaka yako, tuwasiliane kupitia kibuadesigns@gmail.com au jaza fomu upande wa kulia wa blog. Karibuni sana

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...