Hereni za kifuu cha nazi
Wakati wengine wakimaliza kukuna nazi vifuu wanavitupa, wengine wanavitumia hivyo vifuu kutengeneza bidhaa mbalimbali
Miongoni mwa bidhaa hizo ni hizi za urembo
Pichani hapa tuna hereni zilizotengenezwa kwa kutumia vifuu vya nazi.
Lakini si hereni pekee ambazo zinatengenezwa kutokana na vifuu vya nazi, zipo bidhaa nyingine kama mikufu, bangili, upawa wa kuchotea mboga, nk.
Hata wewe hapo nyumbani unaweza kufanya ubunifu huu, ukimaliza kukuna nazi kwa ajili ya chakula chako, basi hifadhi vile vifuu usivitupe kwani vina faida kama tulivyoona hapo juu.
Nawatakieni nyote Jumapili njema yenye utulivu na maandalizi mema ya kuupokea mwaka mpya wa 2013
Nawapenda sana
xoxo
***
Hizi ni hereni ambazo zimesukwa kwa kutumia majani ambayo hutumika kusukia mikeka, makawa, vikapu, nk.
Yapo majani ya aina tofauti tofauti ambayo hutumika kusukia vitu hivyo nilivyovitaja hapo juu
Baadhi ya majani hayo ni ukindu na mlala
Hereni hizi zimesukwa kwa majani ya ukindu ambayo hukaushwa kabla ya kutumika
Hereni hizi ni nzuri kwa kweli na zinapendeza haswa. Chukua hiyo na ujaribu kutupiamo utakubaliana na mimi.
Nawatakieni nyote Weekend Njema yenye amani na furaha tele
xoxo
***