dresses kanga

KANGALICIOUS

1/15/2013Violet Kibua

 
Me, Myself n I

 

 Hivi unajua kwamba kanga nayo yaweza fanya maajabu katika fashion. Kwanza kanga hazina gharama sana, kama vitenge. Hata yule mpenda mitindo wa kipato cha chini kama mimi hapa anaweza kununua kanga na akadesign anavyojua yeye, mwisho wa siku akatokelezea fresh.Ukipata designer mzuri akakupangia yale maua ya kanga vizuri sina shaka utapendeza
 Tatizo la kanga hazina mapana makubwa, kwahiyo mitindo yake mara nyingi inakua simple. Labda kama utataka mtindo wa makorokoro utalazimika kununua doti zaidi ya moja.

Kama mimi hapa nimedesign kamtindo simple, na naamini nimependeza. Hiki kivazi naweza hata vaa ofisini, au mnasemaje wadau wangu?


 
Ni hayo tu niliyo nayo kwa siku ya leo.
Niwatakieni nyote siku njema, tuombe baraka za Mungu ili tuendelee kupeana haya mambo mazuri ya mitindo na urembo.

Kibua V

xoxo

***You Might Also Like

4 comments

 1. kanga imepoa. pendeza wewe

  ReplyDelete
 2. Beautiful dress, love the color.

  xo
  Tiffy
  www.CuteLA.com

  ReplyDelete
 3. Love the dress! Nice fit!


  xoxo
  Nike O.
  www.eighthundredsqft.com

  ReplyDelete

Recent posts

Contact Form