Mahitaji:
Mchele
Choroko
Tui la nazi
Chumvi
Maji
Njia:
Chambua mchele kwa kutoa taka taka zote kisha uoshe vizuri ikiwezekana pembua ili kuondoa mawe kama mchele wako utakua na mawe
Chambua choroko na kisha zioshe vizuri na zichemshe kidogo, zisiive sana kwani zitalainika wakati unapoendelea kupika wali. Kwahiyo uwe makini hapa choroko zisiive
Kuna nazi yako uliyoiandaa
Pasha maji yawe ya uvuguvugu kidogo kwa ajili ya kuandalia tui. Ukitumia maji baridi tui halitoki vizuri, tui la kwanza(tui bubu) liweke pembeni kwani litatumika baadae kadiri unavyoendelea kupika
Endelea kuchuja tui la pili au na la tatu mpaka upate kiasi cha tui linalohitajika kwa pishi lako
Baada ya kuandaa tui lako tayari, weka kwenye sufuria ambayo utatumia kupikia pishi lako
Ongezea na choroko humohumo kwenye tui la nazi
Koroga koroga tui ili lisikatike
Baada ya tui kuchemka, ongezea chumvi na mchele. Koroga kidogo kisha funika ili wali wako uendelee kuiva taratibu
Angalia moto usiwe mkali, uwe wa wastani ili chakula chako kisiungue
Baada ya muda maji yatakua yamekaukia kwenye chakula chako, chukua lile tui bubu ulilokamua mwanzo, ongezea kwenye chakula chako kisha funika
Baada ya dakika kadhaa angalia chakula chako kama maji yatakua yamekaukia geuza chakula chako kisha funika tena
Kisha hapo utakua unageuza geuza chakula chako mpaka uhakikishe kimeiva
Chakula chako kikiiva kitakua na muonekano huu
Hapo kitakua tayari kwa kuliwa
Unaweza kuandaa na mchuzi wa kusindikizia chakula chako, kama mchuzi wa nyama, samaki, salad au ukiamua mbogamboga za majani yote sawa.
Lakini pia unaweza kula hivihivi kwa kuwa hapo tayari ni wali na mboga
Pia unaweza ukaandaa na kinywaji chochote
Una swali, maoni, ushauri?
Au una pishi ungependa kushare nasi
Niandikie kibuafashions@gmail.com
***
Violet
1 comments
Asante sana..imenisaidia
ReplyDelete