mapishi

RAINBOW BEEF

6/08/2013Violet Kibua


Mahitaji: 
Nyama/Beef
Soya sauce
Tangawizi
Kitunguu saumu
Limao/ndimu(sio lazima)
Mafuta ya kupikia
Kitunguu maji
Nyanya
Hoho
Karoti
Chumvi


Njia:
Anza kwa kukatakata nyama, kisha isafishe vizuri. Kisha changanya nyama pamoja na tangawizi na kitunguu saumu ambavyo utakua umeviandaa kwa kuviponda au kuvichop. Ongezea na soya sauce kisha iache kwa muda wa kama dakika 30 mpaka 45. Hii itasaidia nyama kuiva haraka

Wakati unasubiria nyama iendelee kuchanganyika na viungo vizuri, tumia muda huo kuandaa mbogamboga zako ambazo zitaenda sambamba na pishi hili la rainbow beef

Baada ya mahitaji yako yote kuwa tayari, andaaa jiko lako utakalotumia kupikia pishi lako, angalia moto usiwe mkali kwan utasababisha chakula chako kutoiva vizuri

Weka sufuria yako jikoni, ikishapata moto weka mafuta ya kupikia kiasi
Mafuta yakishapata moto, weka nyama na ukoroge koroge mpaka itakapoiva
Nyama ikishaiva vizuri weka mbogamboga zako, anza na vitunguu maji, karoti, hoho kisha malizia na nyanya. Geuza kwa sekunde kadhaa mpaka uone mboga mboga zimechanyanyika vizuri na nyama. Kisha tia chumvi kwa ajili ya taste. 

Usiache mboga mboga zikaiva sana kwani hazitaleta maana ya jina la pishi hili. Kwa kuwa ni rainbow beef lazima mboga mboga zionekane vizuri na rangi zake. Pia katika mahitaji yako waweza kuongezea red pepper, yellow pepper, uyoga nk. kadiri ya mapenzi yako. mimi kwa leo nimetumia mahitaji haya unayoyaona kwenye picha

Baada ya hapo pishi lako linakua tayari kwa kuliwa.Unaweza kuandaa na chakula chochote unachopenda, kama wali, tambi, macaroni, ugali, viazi nk.
Si vibaya kukawa na kinywaji pembeni kama juice au soda

Na hili ndio pishi letu la leo rainbow beef. Unaweza kuandaa wewe mwenyewe hapo nyumbani kwa kufuata njia hizi nilizozielezea

Una swali, maoni, ushauri?
Niandikie kibuafashions@gmail.com

***

Violet

You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form