mapishi

PEPPER STEAK

5/26/2013Violet Kibua

Habari za jumapili wapendwa
Natumai mu wazima wa afya na Mungu bado anatupigania
Tumshukuru kwa upendo wake mkuu

Leo nawaletea pishi hili la nyama(steki) iliyojaa hoho
Kitaalamu tunaita pepper steak

Unataka kujua jinsi ya kuandaa pishi hili?
Tuwe pamoja

Mahitaji:
Nyama(steki)
Limao au Ndimu
Tangawizi
Kitunguu Saumu
Kitunguu maji
Hoho
Mafuta ya kupikia
 Chumvi


Njia:


 Anza kwa kuandaa nyama ambayo ni steki, ikatekate vipande vidogo vidogo
Kisha ioshe vizuri kwa maji safi. Baada ya kuiosha vizuri, tia mchanganyiko wa kitunguu saumu na tangawizi katika nyama, usisahau kuongezea juisi ya limao au ndimu.
Pia kama utapenda si vibaya kuongezea na soya sauce

Uache mchanganyiko wako kwa muda wa kama dk 20 mpaka 30 ili viungo viingie vizuri kwenye nyama. Pia kuacha mchanganyiko huu kwa muda kunasaidia kulainisha  nyama na kuifanya iive haraka wakati wa kupika

Weka jikoni chombo chako ambacho utatumia kupikia pepper steak yako. Iwe ni sufuria, chungu au hata pan itategemea na wingi wa mboga yako
Sufuria ikishapata moto weka mafuta  ya kupikia au ukipenda waweza tumia siagi
Baada ya mafuta kuwa yameshapata moto, weka ule mchanganyiko wako wa nyama na viungo
Geuza geuza kwa muda mpaka nyama iive na kubadilika rangi na kuwa ya kahawia. Kua makini na moto kwani mboga hii inataka ipikwe kwa moto mdogo. Moto ukiwa mkali nyama haitaiva vizuri, itababuka tu

Kisha ongezea vitunguu maji ambavyo utakua umeviandaa na kuvikata katika mtindo wowote utakopendezwa nao. Mimi hapa nimekata cubes
Geuza kidogo, kisha weka hoho na pia usisahau kuongeza na chumvi kiasi kwa ajili ya taste

Geuza geuza kwa sekunde kadhaa hakikisha mboga mboga uliweka yani hoho na vitunguu haziivi sana, kwani ukiacha zikaiva sana utapoteza maana halisi ya jina la mboga hii

Ukiridhika kwamba vimechanganyika vizuri basi epua kwani mboga yako itakua tayari


Taraaaaa..!
Tayari kwa kuliwa
Mimi leo nimeandaa wali, lakini waweza kuandaa chochote utakachopenda wewe ili kiende sambamba na mboga yako

Hilo ndio lilikuwa pishi letu la leo
Endelea kutembelea kijiwe hiki kwa mapishi zaidi

Una pishi lako ungependa kushare nasi
Niandikie
kibuafashions@gmail.com

***

Violet

You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form