african print ankara

KITENGE + SATIN

5/13/2013Violet Kibua
Habari watu wangu!
Mko poa?
Natumai wote mu wazima wa afya njema kabisa
Tumshukuru Mungu wetu kwa kuwa ni mwema, fadhili zake ni za milele
Kwa kutupa pumzi na nguvu ya kuendelea kumtumikia

Leo nawaletea kitu kingine hiki kutoka kwangu. Ni African print(Kitenge) na satin
Sketi ni ya kawaida tu, wenyewe tunaita nguva ya kuunga. Haina vikorombwezo vingi. Nimetumia kitenge pekee

Lakini katika blauzi nimemix, satin imeingia kwa wingi na kitenge kimetia madoido kidogo kwenye kola na upande wa mbele wa vifungo. Kama unavyoona kwenye picha hapo, nimeweka vijimarinda fulani hivi kunogesha tu. 
Blauzi hii ni mtindo wa shati, lakini hii si kama mashati ya kawaida. Hapa utaona tofauti kidogo kwenye mikono. Si kama mikono ya shati za kawaida. Nimetia mbwembwe kidogo.

Hope umeipenda

Nawatakia siku njema na Mungu awe nanyi daima

Asante kwa kunitembelea, Na karibu tena wakati mwingine

***

Violet

You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form