Mahitaji:
Nyama/Steak
Tangawizi
Kitunguu Saumu
Chumvi
Limao/Ndimu
Soy sauce/Sio lazima
Hoho
Karoti
Njia:
Anza kwa kuandaa nyama kwa kuikata kata vipande vidogo vidogo
Kisha andaa kitunguu saumu na tangawizi kwa kuvitwanga au kuvichop
Changanya nyama pamoja na viungo vyako vyote ulivyoandaa, yaani kitunguu saumu/tangawizi, limao au ndimu, chumvi, soy sauce kama utapenda kuitumia, kisha acha kwa muda wa dakika 30 ili viungo vipate kuchanganyika vizuri na nyama
Andaa mbogamboga zako ambazo ni karoti na hoho kwa kuzikata vipande vidogo vidogo
Kisha anza kutunga kwenye spoku au kwenye vijiti maalum vya kuchomea mishikaki
Utakua unachanganya nyama na mboga mboga kadiri utakavyopenda wewe
Baada ya hapo utaanza kuchoma mishikaki yako katika jiko lenye moto wa wastani
Angalia moto usiwe mkali, mishikaki inatakiwa iive taratibu kwenye moto mdogo
Moto ukiwa mkali utasababisha mishikaki ibabuke badala ya kuiva
Ukishahakikisha mishikaki imeiva vizuri, andaa mezani kwa kuliwa
Unaweza kula kwa ugali, chips au chochote utakachopenda wewe
Pia unaweza kula yenyewe kama mlo kamili bila kuongezea chakula kingine
Ni vizuri ukiwa na kinywaji pembeni, kama soda, juice, bia, nk
Hili ndio pishi letu la leo
Kwa wale ambao walikua hawajui namna ya kuandaa mishikaki, naamini post hii itawasaidia
Kama una maoni, ushauri, pengine ungependa kushare nasi pishi la aina yoyote ile
Niandikie, kibuafashions@gmail.com
***
Violet
***
Violet
0 comments