urembo

SCRUB YA NAZI (COCONUT SCRUB)

6/05/2013Violet Kibua


 Habari wadau!

Hivi unajua kuwa unaweza kuwa mrembo kwa kutumia vitu vya asili tu?
Ndio inawezekana! Wengi wetu tumekariri kwamba, ili uwe mrembo na mwenye muonekano wa kuvutia machoni pa watu, basi ni lazima utumie vipodozi vya madukani, vyenye kemikali za kila aina. Tena vingine vina kemikali za sumu. Na vipodozi hivi vinauzwa kwa bei ghali kweli. Na wakati mwingine usipate hata yale matokeo uliyokuwa unategemea. Unakua umepoteza pesa na umezidi kuharibu muonekano wako wa asili.

Kwa nini uendelee kupoteza pesa na muda kwa vipodozi ambavyo havikupi matokeo stahili.
Wakati kuna vitu vya asili ambavyo vinaweza kukusaidia ukawa na muonekano mzuri, tena kwa gharama nafuu

Sasa leo nitawaeleza maajabu ya nazi katika urembo
Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza ikatumika kama scrub kwa ngozi yako

Fuata hatua hizi hapa chini ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako kuwa na muonekano mzuri
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini kwa leo nitaelezea namna ya kuitumia kwa uso wako

 Weninge huwa wanachanganya nazi pamoja na asali, limao, tangawizi, nk. Hii ninayoielezea hapa haijachanganywa na kitu chochote kile. Ni nazi pekee

Nini cha kufanya:
* Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri. Ili upate matokeo mazuri jitahidi kuikuna taratibu ili itoke laini
* Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa(medicated soap)
*Kausha uso wako kwa taulo safi
*Baada ya uso wako kuwa mkavu, chukua ile nazi yako uliyokuna tayari, taratibu anza kusugua usoni kwa dadika kama 3 mpaka 5
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20
*Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida
*Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote


Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yani mara 1 kwa siku. Amini nakuambia utapata matokeo mazuri

Ni hayo tu niliyowaandalia siku ya leo wapendwa wangu

Kama una swali, maoni au ushauri
Niandikie kibuafashions@gmail.com

Pia kama una chochote kizuri cha kushare nasi, usisite kuniandikia

Uwe na siku njema mdau

***

Violet

You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form