mapishi

CHACHANDU

8/17/2013Unknown

Hamjambo!
 Leo tuone jinsi ya kutengeneza chachandu

Mahitaji:
Pilipili kali (inayowasha)
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Sukari (sio lazima)
Kitunguu saumu
Kitunguu maji
Tangawizi
Hoho
Nyanya

Mimi nimetumia pilipili mbuzi
Lakini waweza tumia pilipili aina yoyote inayowasha





 Njia:
 Andaa mahitaji yako yote kama inavyoonekana pichani juu
Kisha weka sufuria jikoni ili ipate moto
Weka mafuta ya kupikia kiasi kulingana na wingi wa pishi lako
Mafuta yakishapata moto, anza kwa kuweka kitunguu maji
Kisha kitunguu saumu na tangawizi ambazo utakua umeziponda au kuzisaga

Baada ya vitunguu vyako kuiva, weka hoho
Kisha ongezea pilipili na nyanya
Acha vichemke kidogo, kabla havijaiva kabisa ongezea chumvi na sukari kiasi kama utapenda
Kisha acha kwa muda ili chachandu ipate kuiva itategemea na moto wako mkali kiasi gani

Baada ya hapo chachandu yako itakua tayari kutumika
Inaenda na vyakula vingi, hususani kwa wale wanaopenda muwasho kwenye chakula
Sio lazima utumie pilipili ya tunda(fresh)
Unaweza kutumia chachandu hii na ukafurahia mlo wako


 Hifadhi kwenye chombo chenye mfuniko kama hivi
Kila mtu ana namna yake ya kuhifadhi chachandu ili isiharibike haraka
Wengine wanaianika juani kwa muda mrefu
Lakini mimi huwa ninahifadhi kwenye friji

Kama una mbinu nyingine mbadala tofauti na friji ya kuhifadhi chachandu ili isiharibike, tujuze ili na wengine wapate kujifunza


Hili ndio lilikua pishi letu la leo
Una maswali, maoni au ushauri?
Au pengine ungependa kujua jinsi ya kuandaa pishi fulani na hujui jinsi ya kuandaa pishi hilo
Usisite, niandikie
kibuafashions@gmail.com

Pia nawakaribisha wote wanaopenda kushare nasi mapishi tofauti tofauti

Asante kwa kunitembelea
Karibu tena

***

Bloglovin  |  Facebook  |  Twitter  |  Instagram  |  Pinterest

Signature photo VIOPYT_zps848f22d6.jpg

You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form