mapishi

FRESH FRUITS SALAD

5/09/2013Violet Kibua

 Kama unapenda kujua ni mchanganyiko wa nini na nini tuwe wote 

Mahitaji:
Parachichi/Avocado
Nanasi/Pineapple
Korosho/Cashewnuts

Njia:
Mchanganyiko huu wala hauna kazi sana kuuandaa
Ukishakuwa na mahitaji yako tayari, Unachotakiwa kufanya
Kwanza kabisa safisha matunda yako vizuri kwa maji safi ya uvuguvugu
Ukishamaliza yaache yachuruzike maji

Baada ya hapo ondoa maganda ya matunda yako uliyoandaa
Ukishamaliza kumenya, katakata matunda yako katika vipande vidogo vidogo jinsi unavyopenda wewe mwenyewe


Baada ya hapo unaongezea na korosho kwa juu, saladi yako inakua tayari kwa kuliwa
Unaweza kuweka saladi yako kwenye friji ili ipoe kidogo
Sio lazima, kama unapenda maana si wote wanaopenda kula vya baridi

Pia sio lazima iwe parachichi na nanasi, unaweza pia kuongeza matunda mengine kadiri upendavyo

Una pishi lako ambalo ungependa kushare nasi ili wengine wajifunze kutoka kwako?
Nitumie email ya pishi lako uliloliandaa na mimi sitasita kuliweka hewani

kibuafashions@gmail.com

 Asante kwa kunitembelea
Karibu tena

***

Violet

You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form