mapishi

TENDE SHAKE

7/05/2013Violet Kibua


Mahitaji:
Tende
Maziwa
Vanilla Ice cream au Vanilla syrup/sio lazima


 
 Njia:
Anza kwa kutoa mbegu kwenye tende
Kisha kata vipande vidogo vidogo

Ukishatoa mbegu na kukata kata, tende zitakua na muonekano kama huu pichani chini
Picha juu, tende kabla ya kutoa mbegu na kukata kata
 
 
Baada ya hapo, chukua mahitaji yako yote, yaani tende, maziwa, vanilla ice cream au syrup kama utapenda kutumia
Weka mahitaji yako yote kwenye blender, kisha saga mpaka itakapokua laini

Pia unaweza ukaloweka tende kwenye maziwa kwa muda, baada ya kuwa umeshaziandaa ili zilainike kwa urahisi wakati wa kusaga kwenye blender


Ukiridhika na ulaini wa shake yako, basi mimina kwenye glass au chombo chochote ulichoandaa, weka kwenye friji kwa muda kidogo, ikishapoa inakua ipo tayari kwa kunywa
Kama hupendi kunywa vya baridi basi sio lazima kuweka kwenye friji, ikishakua tayari mimina kwenye glass na uburudike na kinywaji chako


 Ikiwa tayari kwa kunywa, inakua na muonekano huu


Ni tamu sana
Na shake hii haiitaji kuongeza sukari, kwani tende zenyewe zinakua tayari zina sukari nyingi tu
Na kama utaongezea na vanilla ice cream nayo itakua na sukari pia, kwahiyo ukiongeza tena sukari utapata kitu kitamu zaidi ya asali

Kwa upande wa jikoni, leo niliwaandalia hiyo tende shake

Kama una maswali, maoni, ushauri au una lolote la kushare nami
Niandikie, kibuafashions@gmail.com

***
You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form