Mahitaji:
Mahindi yaliyokobolewa
Maharage
Hoho
Karoti
Kitunguu
Chumvi
Njia:
Anza kwa kuandaa mahindi na maharage kwa kuyachambua na kuyaosha vizuri
Kisha weka katika chombo utakachotumia kupikia, halafu bandika jikoni
Kwakuwa mahindi na maharage yanachukua muda mrefu kuiva, ni muhimu kuweka maji ya kutosha
Na ukiona maji yamekaukia na bado mchanganyiko wako haujaiva vizuri, basi ongeza maji kiasi
Na maji hayo ni vizuri yawe ya moto au uvuguvugu
Andaa mboga mboga zako ambazo ni hoho, karoti na kitunguu, kwa kuvikata vipande vidogo vidogo
Baada ya mchanganyiko wako wa mahindi na maharage kuwa umeiva ongeza chumvi kiasi,
Acha kwa muda kidogo ili mbogamboga zipate kuiva, lakini angalia zisiive sana mpaka zikalainika
Andaa tui la nazi kwa kukamua tui la kwanza na pili
Utaanza kwa kuweka tui la pili, likishachemka kidogo utamalizia kwa kuweka tui la kwanza au tui bubu
Utaacha tui lichemke kwa muda kidogo ili lipate kuiva
0 comments