
Aje! Mko poa? Nyingine hii ya kitenge kutoka kwangu Ni sketi ya belt kubwa, malinda ya kuvuta na mifuko Zipu na vifungo, nimeweka nyuma Ni rahisi sana kutengeneza hii sketi, sababu ya muda nashindwa kupost picha na video za jinsi ya kutengeneza nguo simple ambazo wewe mdau unaweza ukajitengenezea ya kwako hapo nyumbani Naahidi nitakapopata muda nitapost tutorial za kushona nguo simple Sketi kama hii haiitaji uwe mtaalamu...
Mahitaji: Nyama/Beef Soya sauce Tangawizi Kitunguu saumu Limao/ndimu(sio lazima) Mafuta ya kupikia Kitunguu maji Nyanya Hoho Karoti Chumvi Njia: Anza kwa kukatakata nyama, kisha isafishe vizuri. Kisha changanya nyama pamoja na tangawizi na kitunguu saumu ambavyo utakua umeviandaa kwa kuviponda au kuvichop. Ongezea na soya sauce kisha iache kwa muda wa kama dakika 30 mpaka 45. Hii itasaidia nyama kuiva haraka Wakati unasubiria nyama iendelee kuchanganyika na viungo...
Habari wadau! Hivi unajua kuwa unaweza kuwa mrembo kwa kutumia vitu vya asili tu? Ndio inawezekana! Wengi wetu tumekariri kwamba, ili uwe mrembo na mwenye muonekano wa kuvutia machoni pa watu, basi ni lazima utumie vipodozi vya madukani, vyenye kemikali za kila aina. Tena vingine vina kemikali za sumu. Na vipodozi hivi vinauzwa kwa bei ghali kweli. Na wakati mwingine usipate hata yale matokeo uliyokuwa unategemea. Unakua umepoteza...
Mahitaji: Mchele Choroko Tui la nazi Chumvi Maji Njia: Chambua mchele kwa kutoa taka taka zote kisha uoshe vizuri ikiwezekana pembua ili kuondoa mawe kama mchele wako utakua na mawe Chambua choroko na kisha zioshe vizuri na zichemshe kidogo, zisiive sana kwani zitalainika wakati unapoendelea kupika wali. Kwahiyo uwe makini hapa choroko zisiive Kuna nazi yako uliyoiandaa Pasha maji yawe ya uvuguvugu kidogo kwa ajili ya kuandalia tui....