batiki dresses

BATIK SHIRT DRESS

3/09/2013Violet Kibua


Mambo ni aje wadau?
Mko pouwa? Weekend imekaaje?
Natumai wote mu wazima wa afya. Mi niko poa, namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na nguvu tele hata tunaendelea kupeana mambo mazuri kama kawaida.
Baada ya kusherehekea sikukuu yetu kina mama sasa ni wakati wa mapinduzi kwa kina mama wote
tujitume, tuache uvivu wa kukaa bure na kuwategemea kina baba kwa kila kitu. Hii si nzuri ndio maana wamama wengi wananyanyasika kwa sababu tu hana pa kushikilia.

Turudi kwenye kivazi cha leo. 
hiki ni kivazi cha batiki. batiki hii ina rangi za light blue na brown.
Mtindo huu unaitwa shirt dress kibongo bongo tuiite shati gauni.
Ni mtindo ambao unaposhona mikato yake inakua kama ya shati. angalia picha vizuri utaona vifungo vimeshuka kutoka juu mpaka chini. Na shingoni hapo imewekwa kola ya shati. Na ndio maana mtindo huu ukaitwa shirt dress.

Hapa mimi nimeweka mikono ya saizi fulani hivi, sio mirefu sana na wala sio mifupi. Lakini wewe kama umependa mtindo huu na ukaamua kutengeneza ya kwako, basi unaweza ukaweka mkono kwa dizaini yoyote unayopenda wewe sio lazima mkono uwe kama huu nilioweka mimi.
Mi nimetupiamo na belt ndogo ya rangi ya  bluu kuleta mvuto zaidi. 
Naaamini imekuvutia na umeipenda.

Basi, niwatakie weekend njema watu wangu wote
Nawapenda sana. Weekend hii tujiachie kwa amani na utulivu pia kwa kiasi, tukumbuke kuwa kuna kesho

Asanteni sana kwa kutembelea ukurasa wangu
Tuendelee kuwa pamoja kwa mambo mengi mazuri

Mungu awalinde daima

Dress: Kibua Designs
Photos: Jizzle Stans

xoxo

***

Kibua V

You Might Also Like

11 comments

 1. i love the Batik design! And you look stunning
  www.lamodemm.blogspot.co.uk

  ReplyDelete
 2. Hi dear. You look so lovely. Thanks for adding me on IFB sweets.

  xx
  Tanya http://attraction2fashion.com

  ReplyDelete
 3. Hello. Nice meeting you! Looking forward for your next posts. Followed you via GFC. :)

  ReplyDelete
 4. Love this dress! It looks stunning on you. Very nice post! :)

  http://beautifulfreaks17.blogspot.com/

  ReplyDelete

Recent posts

Contact Form