accessories

ZA MPINGO

1/05/2013Violet Kibua


Unaujua  mpingo?

Basi huu ni mti unaopatikana hapa nchini kwetu Tanzania. Ni mti maarufu sana katika sanaa ya uchongaji. Mpingo hutumika kuchonga vitu mbalimbali kama vinyago vya kupamba majumbani, maofisini na sehemu nyingine tofauti tofauti kulingana na muhusika anavyopenda, Vinu vya kutwangia viungo mbalimbali, nk.

Lakini mpingo pia hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali za urembo, kama hapo juu pichani, ni hereni na bangili zilizotengenezwa kwa mti wa mpingo.

Hereni na Bangili hizi ni nzuri sana, kwanza zinadumu kwa muda mrefu kwa sababu mti uliotumika kutengeneza bidhaa hizi ni mti mgumu sana, kwahiyo hazivunjiki kwa urahisi. Pili hazipitwi na wakati, kwasababu mara zote vitu vya asili na kitamaduni huwa vinapendwa

Kama zimekuvutia tafuta yako utupiemo uone jinsi utakavyopendeza.

Ni hayo tu niliyokuandalia kwa siku ya leo. Nawatakia wadau wote weekend njema ya amani, upendo na utulivu wa hali ya juu.

Nawapenda sana

xoxo

***You Might Also Like

0 comments

Recent posts

Contact Form